Thursday, 14 December 2017

Watu wengi wauawa katika shambulio dhidi ya chuo cha polisi Somalia.


mediaShambulio la kujitoa muhanga lagharimu maisha ya watu wengi Mogadishu, Somalia.
Watu wengi wameuawa katika shambulio la kujitoa muhanga lilitokea leo Alhamisi katika chuo cha polisi mjini Mogadishu, nchini Somalia, kwa mujibu polisi.



"Mtu mmoja aliyevalia mkanda wa kulipuka aliingia katika kambi ambako kunapatikana chuo cha polisi, huku akijifananisha na ploisi na kujilipua," afisa wa polisi Mohamed Abdulle alisema, huku akibaini kwamba watu wengi wameuawa bila hata hivyo kutaja idadi.
Kwa mujibu wa mashahidi, polisi wamekua wamekusanyika kwa mazoezi yao ya asubuhi, wakati ambapo mshambuliaji alijilipua.
"Maafisa wa idara ya dharura wanaendelea na zoezi la uokoaji," amesema afisa wa polisi Abdulle.
Kambi iliyoshambuliwa ni sehemu ya shule kubwa ya polisi nchini Somalia.
Mpaka sasa hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na shambulio hilo.
Kundi la Al Shabab, lenye mafungamano na al-Qaeda, limekua likitekeza mashambulizi dhidi ya vikosi vya polisi.
Shambulizi baya zaidi katika historia ya Somalia liligharimu maisha ya watu 512 mnamo Oktoba 14 wakati bomu lililotegwa katika lori bomu lililipuka mjini Mogadishu.
Chanzo:RFI swahil

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...