Rais Magufuli ametengua uteuzi wa wakurugenzi Bukoba.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Bw. Erasto Mfugale na Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Vijijini Bi. Mwantumu Dau wakisubiri kupangiwa kazi.
Taarifa za kutenguliwa kwa Viongozi hao imekuja muda mfupi baada ya Rais kumaliza kuhutubia Bukoba kwenye uzinduzi wa Uwanja wa ndege.
Awali wakati Rais anahutubia alihoji kiasi cha fedha ya mfuko wa barabara kilichopelekwa katika halmashauri hiyo na viopngozi hao wakashindwa kuweka wazi.
No comments:
Post a Comment