Saturday, 20 January 2018
Chama tawala cha ZANU-PF nchini Zimbabwe kimetangaza kuwafukuza wabunge wake 11 ambao ni washirika wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Robert Mugabe
HARARE
Chama tawala cha ZANU-PF nchini Zimbabwe
kimetangaza kuwafukuza wabunge wake 11 ambao ni washirika wa Rais wa
zamani wa nchi hiyo Robert Mugabe.
Maamuzi ya kuvuliwa uanachama
wabunge hao yametolewa na kutangazwa Bungeni na Naibu Spika wa Bunge la
Zimbabwe, Mabel Chinomona baada ya Bunge hilo kupokea barau kutoka kwenye chama
cha ZANU PF iliyosema wabunge hao wamefukuzwa kwa mujibu wa Katiba ya Zimbabwe
kupitia kifungu namba 129 (1) (k).
Naibu Spika amesema kuwa wabunge
waliofukuzwa ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya ndani, aliyekuwa Waziri
wa Nishati, aliyekuwa Waziri wa Michezo, aliyekuwa Naibu Waziri wa Maliasili na
wabunge wengine wa majimbo mbalimbali nchini humo.
Kufuatia zoezi hilo Bunge
limetangaza nafasi wazi katika majimbo hayo 11 na kuijulisha Tume ya Uchaguzi
ya Zimbabwe kuhusu uwepo wa nafasi za wazi katika majimbo hayo kwa mujibu wa
Katiba ya nchi hiyo ili zoezi la uchaguzi liweze kufanyika kupata wawakilishi
wa Wananchi.
Chanzo:Dw swahili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Featured post
MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO
Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio ...

-
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akitembelea Meli hiyo. DAR ES SALAAM Meli kubwa ya Jeshi la Jamhuri ya China yen...
-
MLELE Shule ya msingi kusa iliyopo katika kijiji cha Kanoge kata ya utende Halmashauri ya wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi inatalajia k...
-
NSIMBO Soko la Katumba Mnyaki linalomilikiwa na halamshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi halina choo tangu kuanzishwa kwake hali...
No comments:
Post a Comment