![]() |
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu |
Friday, 19 January 2018
Uagizaji wa dawa nje wagharimu Sh224 bilioni.
DAR ES SALAAM
Serikali
imesema kila mwaka inapoteza mapato ya dola 100 milioni (Sh224 bilioni kwa
kuagiza dawa nje ya nchi.
Akizungumza
katika uzinduzi wa toleo la tano la mwongozo wa matibabu nchini na orodha ya
taifa ya dawa muhimu Waziri wa Afya,
Ummy Mwalimu amesema Serikali itaboresha upatikanaji wa dawa kwa kuimarisha
sekta ya viwanda.
Ummy
ameeleza kuwa kuboreshwa kwa sekta hiyo kutapunguza matumizi ya fedha za kigeni
kuagiza dawa kutoka nje, badala yake kujikita katika kuimarisha uzalishaji wa
dawa kwenye viwanda vya ndani.
Aidha
amefafanua kuwa katika kudhibiti kuenea
kwa usugu wa vimelea vya magonjwa ya kuambukiza, mwongozo umefuata maelekezo
yaliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) ambayo dawa aina ya antibiotiki
zitatakiwa kutumika kwa umakini mkubwa.
Source Mwananchi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Featured post
MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO
Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio ...

-
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akitembelea Meli hiyo. DAR ES SALAAM Meli kubwa ya Jeshi la Jamhuri ya China yen...
-
MLELE Shule ya msingi kusa iliyopo katika kijiji cha Kanoge kata ya utende Halmashauri ya wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi inatalajia k...
-
NSIMBO Soko la Katumba Mnyaki linalomilikiwa na halamshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi halina choo tangu kuanzishwa kwake hali...
No comments:
Post a Comment