Miradi 10 ya maendeleo
yenye thamani ya shilingi milioni 800 imezinduliwa na mwenge wa Uhuru
katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.

Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Chales Kabeho amewataka wananchi
kutumia vizuri miradi iliyo zinduliwa
ili idumu kwa muda mrefu na maslahi ya jamii.
Katika hatua nyingine ameiasa jamii kupinga kwa pamoja mimba za utotoni
ambazo zinakatisha ndoto za wanafunzi.
Mbio za mwenge mwaka huu zinaoongozwa na
kauli mbiu ya elimu ni ufunguo wa maisha wekeza sasa kwa maendeleo ya
Taifa.
Chanzo:Mpanda Radio
No comments:
Post a Comment