Monday, 17 July 2017

WAMILIKI WA VITUO VYA MAFUTA YA PETROL,DIZEL NA MAFUTA YA TAA MKOANI KATAVI WAMETII AGIZO LA SERIKALI KUNUNUA MASHINE ZA KIELEKTRONIKS.

WAMILIKI wa vituo vitano vya mafuta ya Petrol,Dizel na Mafuta ya taa Mkoani Katavi,wametii agizo la serikali linalowataka kununua mashine za kielektroniks(EFDs).

Hatua hiyo imethibitishwa leo na Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Mkoani Katavi Bw.Michael Temu,wakati akizungumza na Mpanda Radio Ofisini Kwake.

 Wakati serikali ikitaka kila anayeuza na kununua risiti itolewe,bado kuna makundi ambayo pengine kutokana na uharaka kikazi au kutoelewa umuhimu wa kudai risti,kwao kudai risiti inaonekana ni kupoteza muda kama ambavyo baadhi leo wamebaisha wakati wakihojiana na Mpanda Radio.

 Katika hatua nyingine,Bw.Temu amesema,kwa mjibu wa kifungu cha sheria namba 38,muuzaji na mnunuzi wanatakiwa kulipa faini hadi shilingi milioni nne ikiwa itathibitika kuwa hakuna risiti iliyotolewa baada ya manunuzi.

 Wiki iliyopita,mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Katavi,ilivifungia vituo vyote vinavyouza mafuta ambapo kwa sasa biashara ya mafuta inaendelea baada ya wamiliki wa vituo hivyo kuafikiana na serikali kuhusu matumizi ya mashine za EFDs.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...