![]() |
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile |
Tuesday, 9 January 2018
Serikali imeviagiza vyombo vya usalama na kamati za Afya za vijiji kuimarisha mifumo ya udhibiti wa upotevu wa Dawa nchini.
Serikali imeviagiza vyombo vya usalama na kamati
za Afya za vijiji kuimarisha mifumo ya udhibiti wa upotevu wa Dawa nchini, ili
kuondoa ubadhilifu unaofanywa na baadhi ya watumishi wasio waaminifu.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile
katika ziara yake Wilaya ya Uvinza
Mkoani Kigoma ya kukagua utoaji huduma za Afya na kufuatilia utekelezaji wa
Sera ya Maendeleo ya jamii .
Katika kupunguza vifo vya kina mama na watoto
Dkt. Faustine amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto imewekeza kiasi cha shilingi Milioni 400 katika
Halmashauri 175, kikiwemo kituo cha Afya cha Uvinza.
Nae Mkuu
wa Wilaya ya Uvinza Bi Mwanamvua Mlindoko ameeleza faida ya mradi wa ujenzi wa
madarasa ikiwemo ongezeko la ufaulu kutoka wanafunzi 4115 mwaka 2017 huku
waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza ni wanafunzi 1641 ambao ni sawa na
asilimia 36.
Chanzo:Mwananchi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Featured post
MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO
Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio ...

-
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akitembelea Meli hiyo. DAR ES SALAAM Meli kubwa ya Jeshi la Jamhuri ya China yen...
-
MLELE Shule ya msingi kusa iliyopo katika kijiji cha Kanoge kata ya utende Halmashauri ya wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi inatalajia k...
-
Kibao cha shule ya msingi nsanda iliyopo katumba B Shule ya msingi nsanda iliyopo kata ya kanoge halmashauri ya nsimbo mkoan katavi ...
No comments:
Post a Comment