Tuesday, 9 January 2018
Msemaji wa Umoja wa Mataifa Bw Stephane Dujarric amesema takriban watu 700 wamepoteza makazi yao kutokana na operesheni za kijeshi dhidi ya waasi wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Kundi la IS zilizofanyika mjini Kirkuk, Iraq tangu Alhamisi iliyopita.
BAGHDAD
Msemaji wa Umoja wa Mataifa Bw Stephane Dujarric
amesema takriban watu 700 wamepoteza makazi yao kutokana na operesheni za
kijeshi dhidi ya waasi wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Kundi la IS
zilizofanyika mjini Kirkuk, Iraq tangu Alhamisi iliyopita.
Msemaji huyo amesema Ofisi ya uratibu wa misaada
ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OCHA imeripoti kuwa watu hao waliokimbia
mapambano kwenye eneo la Hawija wanahamishiwa kambi ya wakimbizi iliyoko karibu
na Daquq, ambako watapewa msaada wa kibinadamu.
Msemaji huyo pia ameongeza kuwa utoaji wa
misaada ya kibinadamu katika eneo la Hawija umesimamishwa kutokana na sababu za
usalama, na utarejeshwa mara baada ya operesheni ya kijeshi kukamilika.
Chanzo: Dw swahili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Featured post
MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO
Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio ...

-
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akitembelea Meli hiyo. DAR ES SALAAM Meli kubwa ya Jeshi la Jamhuri ya China yen...
-
MLELE Shule ya msingi kusa iliyopo katika kijiji cha Kanoge kata ya utende Halmashauri ya wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi inatalajia k...
-
Kibao cha shule ya msingi nsanda iliyopo katumba B Shule ya msingi nsanda iliyopo kata ya kanoge halmashauri ya nsimbo mkoan katavi ...
No comments:
Post a Comment