MPANDA
Baadhi ya WaKazi Mkoani Katavi wameelezea kupanda kwa bei za bidhaa mbali mbali ikiwemo vyakula katika msimu huu wa sikukuu .
Wakizungumza na Mpanda redio fm kwa nyakati tofauti wamesema wafanya biashara huutumia msimu huo kama sehemu ya kujinufaisha na kuwaumiza watu wa kipato cha chini.
Lakini wafanyabiashara wengi wanadai kuwa tatizo la upandishaji wa bei kiholela katika msimu wa sikukuu hufanywa na wafanyabiashara wakubwa kwa hiyo wao hukosa namna.
Mara kwa mara serikali imekuwa ikizitaka mamlaka zinazo husika na udhibiti wa mfuko wa bei kiholela kuchukua hatua za kisheria kwa wafanyabiashara wanao kumbwa na kadhia hiyo.
Chanzo: EATV.
No comments:
Post a Comment