
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuongoza waombolezaji kuaga miili ya askari 14 waliouawa na waasi wa ADF nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Shughuli ya kuaga miili ya askari hao itakayofanyika kesho Alhamisi Desemba 14,2017 saa mbili asubuhi katika viwanja vya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Upanga jijini Dar es Salaam. Pia, itahudhuriwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo.
Taarifa ya leo Jumatano Desemba 13,2017 ya kurugenzi ya habari na uhusiano makao makuu ya Jeshi imesema wengine watakaohudhuria shughuli hiyo ni wakuu kamandi za anga, maji, nchi kavu na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Pia, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, askari na wananchi.
Taarifa hiyo imesema baada ya kukamilika shughuli ya kuaga miili hiyo itasafirishwa kwao mazishi.
Chanzo :mwananchi
No comments:
Post a Comment