KATAVI
Zaidi ya wanafunzi 9000 waliofanya mtihani wa
kumaliza elimu ya msingi mkoani Katavi wamekosa nafasi ya kuingia kidato cha
kwanza kwa mwaka 2018 kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa.
Akitangaza
matokeo ya mtihani huo katika kikao maalumu cha uchaguzi wa wanafunzi Afisa
Elimu mkoa wa Katavi Ernest Hinju amesema jumla watahiniwa 7,190 wamechaguliwa
kujiunga na shule za sekondari za kutwa.
Aidha
watahiniwa 162 hawakuweza kufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali hali
iliyopelekea wadau wa elimu kujadili changamoto za kushuka kwa
elimu, kwani kulinganisha na mwaka uliopita mkoa wa Katavi umeshika nafasi
ya 9 kitaifa kutoka nafasi ya 2 mwaka uliopita
Kwa
upande wake Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Katavi Bwana Gideon Marandu amezitaka
halmashauri zote kuhakikisha wanafunzi waliokosa nafasi wanapata nafasi ifikapo
Februari mwaka 2018.
SOURCE: EATV.
No comments:
Post a Comment