Thursday, 18 January 2018
Marekani jana imetangaza kuwa itazuia kiasi cha dola milioni 65 zilizokuwa zimepangwa kulifadhili shirika la Umoja wa mataifa linalowahudumia wakimbizi wa Palestina la UNRWA.
WASHINGTON
Marekani
jana imetangaza kuwa itazuia kiasi cha dola milioni 65 zilizokuwa zimepangwa
kulifadhili shirika la Umoja wa mataifa linalowahudumia wakimbizi wa Palestina
la UNRWA, wiki mbili baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutishia malipo ya
baadaye.
Wizara hiyo imesema Marekani itatoa dola
milioni 60 kati ya milioni 125 zilizopangwa awali, lakini zilizobaki zitazuiwa
kwa sasa.
Maafisa
wa Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani wamesisitiza uamuzi huo haukuchukuliwa
ili kuwashinikiza viongozi wa Palestina, lakini kwa sababu Marekani inataka
nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Mataifa zisaidie kulipa na kurekebisha
shirika la UNRWA.
Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema hakuwa na taarifa ya uamuzi
huo wa Marekani, lakini taarifa alizozisikia zimempa wasiwasi sana.
Chanzo:Bbc swahili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Featured post
MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO
Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio ...

-
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akitembelea Meli hiyo. DAR ES SALAAM Meli kubwa ya Jeshi la Jamhuri ya China yen...
-
NSIMBO Soko la Katumba Mnyaki linalomilikiwa na halamshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi halina choo tangu kuanzishwa kwake hali...
-
Kibao cha shule ya msingi nsanda iliyopo katumba B Shule ya msingi nsanda iliyopo kata ya kanoge halmashauri ya nsimbo mkoan katavi ...
No comments:
Post a Comment