Thursday, 18 January 2018
Viongozi 18 wa chama cha ACT-Wazalendo kutoka mikoa mbalimbali nchini wamejivua nyadhifa zao na kujiunga na CCM.
MOSHI
Viongozi 18 wa chama cha
ACT-Wazalendo kutoka mikoa mbalimbali nchini wamejivua nyadhifa zao na kujiunga
na CCM.
Viongozi hao wamepokelewa leo
Januari 17, 2018 mjini Moshi na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey
Polepole na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira ambaye hivi karibuni
alihamia chama tawala. Mghwira amewahi kuwa mwenyekiti wa ACT.
Miongoni mwa wanachama hao, wapo
waliokuwa wajumbe wa kamati kuu, wenyeviti wa mikoa na makatibu wa ACT.
Pia, viongozi 18 wa Chadema ngazi
za kata na vijiji kutoka Wilaya ya Siha nao wamejiunga na CCM.
Akizungumzia baada ya
kuwakaribisha, Polepole amesema katika kipindi cha miaka miwili ya utawala wa
Serikali ya Awamu ya Tano, CCM kimeongeza wanachama zaidi ya milioni mbili.
Chanzo: Zanzibar
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Featured post
MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO
Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio ...

-
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akitembelea Meli hiyo. DAR ES SALAAM Meli kubwa ya Jeshi la Jamhuri ya China yen...
-
NSIMBO Soko la Katumba Mnyaki linalomilikiwa na halamshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi halina choo tangu kuanzishwa kwake hali...
-
Kibao cha shule ya msingi nsanda iliyopo katumba B Shule ya msingi nsanda iliyopo kata ya kanoge halmashauri ya nsimbo mkoan katavi ...
No comments:
Post a Comment