DODOMA
Friday, 12 January 2018
Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Mwakisebe kata ya Kimaha wilayani chemba mkoani Dodoma amefariki dunia, huku watu wengine zaidi ya 2000 wakiwa hawana mahali pa kuishi kufuatia mvua mvua kubwa inayo endelea kunyesha.
Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Mwakisebe kata ya
Kimaha wilayani chemba mkoani Dodoma amefariki dunia, huku watu wengine zaidi
ya 2000 wakiwa hawana mahali pa kuishi kufuatia mvua mvua kubwa inayo endelea
kunyesha.
Inadaiwa
kwamba athari za mvua zimejitokeza katika vijiji vya Olboloti ,Kaloleni na
Mrijo Chini ambavyo ndivyo vinavyodaiwa kuathiriwa zaidi na mafuriko hayo, na
kwamba shughuli za uokozi zikiendelea .
Aidha
Mwenyekiti wa kijiji cha Olboloti, Abdallah Suti amesema mvua iliyonyesha
katika maeneo yao ni kubwa na kwamba haijawahi kutokea tangu miaka ya 1960.
Kwa
upande wake Mkuu wa Zimamoto na uokoaji kituo cha Dodoma Amiry Issa amesema
kikosi kinaendelea na shughuli za uokozi kuzunguka vijiji hivyo huku akiwataka
wananchi kutosogelea maeneo hatarishi.
Naye
Mkuu wa wilaya ya Chemba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na
Usalama Wilaya hiyo, Simon Odunga amewataka wananchi waliojenga katika maeneo
ya mabondeni kuhama mara moja.
Chanzo:Eatv
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Featured post
MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO
Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio ...

-
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akitembelea Meli hiyo. DAR ES SALAAM Meli kubwa ya Jeshi la Jamhuri ya China yen...
-
NSIMBO Soko la Katumba Mnyaki linalomilikiwa na halamshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi halina choo tangu kuanzishwa kwake hali...
-
KIGOMA . VITUO vya afya Uvinza na Nguruka vilivyopo wilayani Uvinza Mkoa wa Kigoma vinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo yaup...
No comments:
Post a Comment