Wednesday, 10 January 2018
Wapiganaji zaidi ya 107 wa kundi la Boko Haram wameuawa katika operesheni ya jeshi la Nigeria.
ABUJA
Wapiganaji zaidi ya 107 wa kundi la Boko Haram
wameuawa katika operesheni ya jeshi la Nigeria, miongoni mwao zaidi ya 50
wameuawa karibu na ziwa Chad na wengine zaidi ya 57 wameuawa kwenye eneo la
Metele la jimbo la Borno nchini Nigeria.
Msemaji wa jeshi la Nigeria Bw. Sani Usman
ametoa taarifa akisema lengo la operesheni hiyo ni kuondoa wapiganaji wa kundi
hilo waliosalia katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Msemaji huyo ameongeza kwamba askari wanne wa
jeshi la Nigeria na raia mmoja anayejitolea pia wameuawa kwenye operesheni
hiyo, baada ya deraya walilokuwa wakisafiria kugongwa na gari lenye mabomu ya
kienyeji lililoendeshwa na wapiganaji wa kundi hilo.
CHANZO: DW SWAHILI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Featured post
MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO
Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio ...

-
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akitembelea Meli hiyo. DAR ES SALAAM Meli kubwa ya Jeshi la Jamhuri ya China yen...
-
MLELE Shule ya msingi kusa iliyopo katika kijiji cha Kanoge kata ya utende Halmashauri ya wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi inatalajia k...
-
Kibao cha shule ya msingi nsanda iliyopo katumba B Shule ya msingi nsanda iliyopo kata ya kanoge halmashauri ya nsimbo mkoan katavi ...
No comments:
Post a Comment