Friday, 4 August 2017

Jopo la kuchunguza tuhuma za Urusi labuniwa Marekani.

Robert Mueller kulia ambaye  aliwahi kuhudumu kama mkurugenzi wa FBI ambae anasimamia jopo hilo.
Baraza maalum linalochunguza tuhuma za Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani mwaka jana linaarifiwa kuunda jopo kuu.
Gazeti la The Wall Street Journal linasema jopo hilo kuu la Robert Mueller limeanza kazi katika wiki za hivi karibuni na limewasilisha agizo la kukusanya ushahidi kuhusu mkutano wa Juni mwaka jana kati ya mwanawe rais Trump na wakili mmoja wa Urusi.


 Vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti kuwa uchunguzi wa Robert Mueller'umechukua hatua ya kwanza kuelekea ufunguzi wa mashtaka ya uhalifu. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters , jopo hilo la mahakama limewaita mashahidi kuzungumzia juu ya mkutano wa mwezi Juni mwaka 2016 baina ya mtoto wa kiume wa rais Donald Trump .

 Trump Jr na wakili wa Urusi. Rais Trump anapinga madai yoyote kwamba maafisa wake walikula njama na serikali ya Urusi ili kumshinda Bi Hillary Clinton katika uchaguzi wa urais. Nchini Marekani , jopo kubwa la mahakama huundwa kwa ajili ya kuchunguza ikiwa ushahidi uliopo ni wa kutosha kiasi cha kufungua kesi ya mashtaka ya uhalifu.

 Jopo kubwa la mahakama hata hivyo haliamui juu ya kutokuwepo na hatia wala uwezekano mtu kuwa na hatia. Taarifa ya kwamba jopo kubwa la mahakama limekuwa likikutana mjini Washington DC, na kwamba linachunguza mkutano wa June 2016 baina ya Donald Trump Jr na raia wa Urusi, ni wazi kwamba uchunguzi sasa unaelekezwa kwa wandani wa rais.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...