pichani mtuhumiwa Malandu Likwaja akisubiri hukumu ya kesi yake
Mahakama kuu kanda ya sumbawanga mkoani Katavi imemhukumu adhabu
ya kunyongwa hadi kufa Malandu Likwaja mwenye
umri wa miaka 42 mkazi wa igalula Wilayani
Mlele kwa kosa la kuua kwa kukusudia.
Mwendesha mashtaka wa serikali Lugano mwasubila
mbele ya Jaji Dr Adamu Mambi ameiambia mahakama kuwa mshtakiwa alitenda kosa
hilo Tarehe 13 mwezi wa saba mwaka 2007 ambapo alimuua Ibrahimu Juma kwa kumkata
kwa shoka sehemu za kichwani na shingoni
Mahakama ya hakimu mkazi ilikotolewa hukumu ya mshitakiwa malandu
Aidha Jaji Dr Adamu Mambi amemhukumu kunyongwa hadi kufa kwa mujibu wa kifungu cha 195 na 196 cha sheria ya kanuni za adhabu
sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002 na kubainisha kuwa kilichomtia hatiani ni
kifungu cha 26 kifungu kidogo cha kwanza.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari
amezindua ndege inayojiendesha yenyewe bila ya rubani ambayo ni ya kwanza
kutengenezwa nchini humo.
Kifaa hicho kilichotengenezwa na
Taasisi ya Teknolojia ya jeshi la anga la Nigeria, kitatumika kupambana na
wapiganaji pamoja na majambazi.
Mipango ya jeshi la nchi hiyo ni
kutengeneza vifaa hivyo kwa wingi na pia uwezekano wa kuvisafirisha katika nchi
nyingine.
Nigeria imekuwa ikikabiliwa na
kitisho cha usalama, ikiwemo wapiganaji wa kiislamu walioko kaskazini mwa nchi
hiyo, wapiganaji walioko katika eneo lenye utajiri wa mafuta, kusini mwa nchi
na mapigano kati ya wafugaji na wakulima katika jimbo la kati mwa nchi hiyo.
Kiongozi wa Chama tawala
nchini Afrika kusini cha ANC Cyril Ramaphosa amethibitisha kuwa chama kitafanya
uamuzi wa mwisho juu ya hatma ya Rais Jacob Zuma.
Akizungumza kaika mkutano wa
hadhara mjini Cape Town, Ramaphosa amedokeza kuwa Rais Zuma atatakiwa
kujiuzulu.
Amesisitiza kuwa wala rushwa
wote wanatakiwa kufikishwa katika vyombo vya sheria, kitu ambacho anasema
Nelson Mandela, baba wa taifa hilo angekitaka.
Bwana Ramaphosa alikuwa
akizungumza katika kumbukumbu ya miaka 28 toka Rais wa kwanza mzalendo nnchini
humo Nelson Mandela alipolihutubia taifa, mara tu baada ya kuachiwa gerezani.
Martin Schulz amekataa kuchukua wadhifa wa waziri wa mambo ya kigeni katika serikali mpya itakayoongozwa na kansela Merkel ambayo baada ya kufikia makubaliano kuundwa serikali hiyo wiki hii.
Martin Schulz, kiongozi anayeondoka madarakani katika chama cha Social Democratic SPD nchini Ujerumani, hatachukua wadhifa wa waziri wa mambo ya kigeni aliopewa katika serikali mpya ya Ujerumani, akisalim amri kwa mbinyo mkubwa kutoka ndani ya chama chake kabla ya kura muhimu inayotarajiwa kupigwa na chama cha SPD kuhusiana na makubaliano yaliyofikiwa ya kuunda serikali ya mseto na kansela Angela Merkel.
"Natangaza kwamba sitajiunga na serikali ya muungano na wakati huo huo napenda kutoa matumaini yangu kwamba hali hii itamaliza mjadala unaonihusu ndani ya chama cha SPD," Schulz alisema katika taarifa siku ya Ijumaa(09.02.2018). Schulz amekabiliwa na mapambano ndani ya SPD kwa kukubali kwake kuchukua wadhifa huo wa juu wa kidiplomasia baada ya kuahidi kwamba hatakuwa sehemu ya baraza la mawaziri la Merkel.
Tangazo hilo jana Ijumaa lilikuwa ni pigo jingine kwa rais huyo wa zamani wa bunge la Umoja wa Ulaya mwenye umri wa miaka 62, ambaye siku mbili zilizopita alitangaza kuwa anajiuzulu kuwa kiongozi wa chama cha SPD na kumkabidhi madaraka hayo kiongozi wa wabunge wa chama hicho Andrea Nahles.
Hatua hiyo pia inakuja chini ya wiki mbili kabla ya kura itakayopigwa na wanachama 463,723 wa chama cha SPD juu ya iwapo kujiunga ama kutojiunga na serikali ya muungano itakayoongozwa na Merkel.
Schulz alikuwa amechaguliwa mwaka mmoja uliopita kwa asilimia 100 kukiongoza chama hicho cha siasa za wastani za mrengo wa kushoto. Aliwasili kama shujaa katika medani ya kisiasa nchini humo Januari mwaka jana, akiahidi kwamba atamwangusha Merkel kama kansela na kukiongoza chama cha SPD katika ushindi.Aliwasili kama shujaa
Baada ya kupanda kwa haraka katika uchunguzi wa maoni ya wapiga kura , uchunguzi wa maoni hayo ulionesha uungwaji mkono wa kile vyombo vya habari vya Ujerumani ilichokieleza kuwa ni treni ya Schulz inayopungua nguvu kwa haraka kabla ya kukiongoza chama hicho kufikia kipigo cha kihistoria mwezi Septemba.
Baada ya hapo alifanya makosa kadhaa makubwa ya kisiasa. Kwanza aliondoa kabisa uwezekano wa kuunda muungano mpya na Merkel na baadaye akakataa kabisa kujiunga na baraza lake la mawaziri.
Miezi michache baadaye alilazimika kufuta uamuzi wake wa kujiunga tena pamoja na Merkel baada ya kuvunjika kwa mazungumzo ya kuunda serikali mwezi Novemba na chama cha walinzi wa mazingira pamoja na kile kinachopendelea biashara cha Free Democrats FDP.
Uungwaji mkono waporomoka
Baada ya kupata asilimia 20.5 tu ya kura katika uchaguzi wa mwezi Septemba , uungwaji mkono wa chama cha SPD ulishuka hadi asilimia 17, kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni ya wapiga kura uliochapishwa wiki hii, ambapo asilimia 72 ya wale walioulizwa wanapinga Schulz kujiunga na serikali mpya.
Kiongozi muhimu wa kundi la SPD limemtaka Sigmar Gabriel kubakia kuwa waziri wa mambo ya kigeni baada ya Schulz kuachana na mipango yake ya kuchukua wadhifa huo.
Sigmar Gabriel anapaswa kubakia kuwa waziri wa mambo ya kigeni. "Bila hivyo sitaelewa kitu", aliandika katika ukurasa wa Twitter Johannes Kahrs, mbunge wa chama cha SPD na msemaji wa kundi la wabunge wa chama hicho bungeni, kundi linalojulikana kama Seeheimer. "Uamuzi wa Martin Schulz unapaswa kutambuliwa na anastahili heshima ya juu kabisa," alisema Andrea Nahles.
Image captionMagaidi Alexanda Kotey na El Shafee Elsheikh
Taarifa zinasema kuwa raia wawili wa Uingereza wanaodhaniwa kuwa wanachama wa kikundi cha wapiganaji wa Kiislam cha IS wanashikiliwa na kundi la wapigaji wa Kikurd.
Alexanda Kotey mwenye umri wa miaka 34 na mwenzake El Shafee Elsheikh mwenye miaka 29 ni miongoni mwa vijana wawili waliokuwa wanasakwa kati ya wenzao ambao walikwisha kukamatwa.
Kundi hili la vijana wanne kutoka raia wa Uingereza ndani ya kundi la IS walikuwa ni kundi hatari linalofahamika kama Beatles hiyo ikiwa ni kutokana na lafudhi yao wanapozungumza.
Maofisa wa Marekani wamesema kuwa kundi hilo lililokuwa likihusika na utoaji mateso pamoja na kuua ndani ya IS linadaiwa kuwachinja Zaidi ya watu 27 mateka kutoka nchi za kimagharibi na kutoa mateso makali kwa wengine wengi tu.
Beatles ni akina nani hasa?
Hawa ni kundi hatari kwaajili ya mauaji na mateso,ambalo lilikuwa linajumuisha watu kama Mohammed Emwazi almaarufu kama Jihadi John ambaye alikuwa akionekana katika picha za video akiwa anachinja watu.Aliuawa katika mashambulizi ya anga mwaka 2015 katika mji wa Raqqa ngome ya zamani ya IS.
Lakini wapo pia Aine Davis ambaye naye alikuwa akitokea Uingereza,alihukumiwa baada ya kubainika kuwa alikuwa mmoja wa viongozi waandamizi wa kundi la Islamic State na alifungwa mwaka jana huko Uturuki.Wengine wanaounda kundi hili la Beatles ni Alexanda Kotey ambaye naye anatoka London magharibi,yeye alikuwa katika kitengo cha utesaji,kwa mjibu wa Marekani na alikuwa mtu anaye toa usajili kwa wanaojiunga na IS.
El Shafee Elsheikh huyu yeye ni miongoni mwa waliokuwa wakiunda genge hili,hawa ndiyo Beatles.
Huduma za serikali ya Marekani zimekwama baada ya bunge la Congress
kushindwa kupitisha mkakati muhimu wa bajeti yake kwa wakati unaofaa.
Wabunge walitumai kwamba watapitisha matumizi mapya kabla ya muda wa
kufadhili bajeti hiyo kukamilika.
Lakini seneta wa Republican Rand Paul alimaliza matumaini ya kupigwa kwa
kura ya haraka wakati alipoitisha mjadala bungeni kuhusu marekebisho ya
matumizi.
Mnamo mwezi Januari , kisa kama hicho cha kushindwa kupitisha matumizi ya
serikali katika wakati unaofaa kilisababisha serikali kuwa na mkwamo wa siku
tatu.
Hata hivyo wafanyikazi wa serikali wameombwa kutumia maajenti wa nyumbani
ili kupata ,mwelekeo kuhusu ni lini watarudi kazini.
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya kupitia NASA, Raila Amollo Odinga
NAIROBI
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya kupitia NASA, Raila Amollo Odinga,
ametaka kufanyika kwa uchaguzi mkuu mpya tena mwezi Agosti mwaka huu 2018.
Raila Odinga amesema hamtambui Uhuru Kenyatta kama Rais wa nchi hiyo
kwani hana kibali cha watu, ingawa hana lengo lolote la kupambana na serikali
ya Kenyatta.
Hivi karibuni kiongozi huyo wa upinzani nchini Kenya alijiapisha na kuwa
Rais wa watu, akisema yeye ndio chaguo la watu kuwaongoza na sio Uhuru
Kenyatta.
Haki miliki ya pichImage captionRais Mohamed Abdullahi Farmaajo
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi al maarufu Farmaajo hii leo amefikisha mwaka mmoja tangu achaguliwe.
Mtihani wake mkubwa ungali ni hali ya usalama, huku wapiganaji wakiendelea kufanikisha mashambulio jijini Mogadishu na kwingineko nchini.
Mwezi mitano tu iliyopita, mlipuko wa bomu ya lori iliwaua watu wasiopungua mia tano, kwenye shambulio lilokuwa hatari zaidi katika historia ya nchi hiyo.
Kwenye makutano ya barabara katika soko la Zoobe jijini Mogadishu, biashara imenoga huku na kule. Lakini wengi wa wachuuzi na wauzaji hapa ni waathiriwa wa mkasa wa bomu uliokuwa hatari zaidi katika historia.
Mmoja wao ni Abdifittah Ahmed, mwenye umri wa miaka 28 na na anayemiliki duka la dawa. Uso wake una makovu mawili; moja unapunda kovu la uso wake, linguine linaanzia mdomoni hadi chini ya sikio lake la kushoto. Huku tukitembea barabarani, anakumbuka jinsi alivyojikokota kutoka vifusi vya duka lake.
Image captionAbdifittah Ahmed
Bomu hilo iliporomosha jumba la gorofa mbili alimokuwa akifanyia mauzo.
'Niliivuka barabara hii nikiwa natokwa na damu kichwani, niliiona miili ya watu ikiwa imezagaa barabarani, wengi wakiwa na majeraha, wengine wamepoteza sehemu zao za mwili, wengine wamepoteza fahamu.
'Sikuweza kuona vizuri kwasbabu damu ilikuwa inatiririka kutoka machoni mwangu, lakini bado naona nilikuwa na bahati, kwasababu nilichokiona ilikuwa hali mbaya mno', amesema Abdifittah
Haki miliki ya pichaImage captionMwanaume mmoja akihuzunika karibu na maiti katika eneo ambapo bomu lililipukia jijini Mogadishu Oktoba 14, 2017
Aliwapoteza marafiki wengi siku hiyo. Uharibifu uliosababishwa na mlipuko huo ulienea kwa mamia ya hatua, na kuwaacha wengi wakiwa wamekufa au kujeruhiwa.
Kwa sasa ni vigumu kutambua yaliotokea katika enoe hilo unapotembea. Huwezi kutambua kwamba hapa ndipo watu wengi walipoteza maisha yao miezi mitano iliyopita.
Majengo mengi yamejengwa upya, barabara imetengenezwa, na wafanyabiashara wanaendelea na shughulia zao kama kawaida.
Image captionKikosi maalumu cha jeshi kimeimarisha ukaguzi wa magari haswa nyakati za jioni
Watu wameamua kuendelea na maisha yao kana kwamba hakuna kilichotokea. Lakini akilini mwao shambulio hilo limewacha kovu na kumbukumbu zitakazodumu maisha.
Miezi michache baada ya kutwaa urais wa Somalia kutoka uwanja wa ndege kwa kuhofia mashambulio ya Al Shabaab, Mohamed Abdullahi alitoa ahadi yake kwa wananchi wa Somalia.
Alisema, 'Lengo langu ni kuwashinda Al Shabaab kwa miaka miwili ijayo. Natumai kwamba tukifanya kazi pamoja, tutaleta Amani na utulivu nchini Somalia'.
Lakini uongozi wake umeshuhudia mashambulio, na Mogadishu ingali mojawapo wa miji hatari zaidi duniani.
Wachanganuzi wanaamiini kuwa jinamizi la Al Shabab ni gumu kuliangamiza..
Hassan Sheikh, ni mchambuzi wa masuala ya usalama anasema, 'Kwa sababu ni wapiganaji, wanaweza kupenya kirahisi katika maeneo ya umma na ya kibinafsi, na wana athari kubwa katika mfumo wa jamii kisiasa, kiuchumi na kijamii.
'Muhimu zaidi ni kuwa walisababisha uoga, na uoga huu huwasaidia kwani ni vigumu sana kuwakamata au kuwashinda'.
Barabarani, kikosi maalumu cha jeshi kimeimarisha ukaguzi wa magari haswa nyakati za jioni; huku magari karibu yote yakisimamishwa na kukaguliwa vikali pamoja na abiria.
Wakazi wanatumai kwamba hatua hizi zitaweza kurejesha matumaini yao ambayo kwa sasa yako gizani.
Haki miliki ya pichaImage captionMagwaride ya kijeshi ya hapo awali yamekuwa yakionyesha uwezo wa kijeshi
Taifa la Korea Kaskazini linatarajiwa kuandaa maadhimisho ya 70 ya gwaride la jeshi lake kabla ya kufanyika kwa michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi nchini Korea Kusini.
Gwaride la kila mwaka la Pyongyang linaloadhimisha kuanzishwa kwa jeshi la Korea Kaskazini limekuwa likifanywa kila mwezi Aprili kwa kipindi cha miaka 40.
Hatahivyo vyombo vya habari nchini humo vilitangaza mapema mwaka huu kwamba tarehe ya kufanyika kwa gwaride hilo la kijeshi imebadilishwa hadi Februari 8.
Korea Kaskazini imepuuzilia mbali ukosoaji wa mpango wake ikisema kuwa hakuna mtu aliye na uwezo wa kuishutumu.
''Ni utamaduni na swala muhimu sana kwamba kila taifa duniani linasherehekea uzinduzi wa jeshi lake' , kilisema chama tawala cha wafanyikazi Rodong Sinmun.
Haki miliki ya picImage captionNi jambo la kawaida kwa Korea Kaskazini kufanya gwaride la kijeshi
Marekani imesema kuwa ingependelea gwaride hilo kutofanyika kwa kuwa kwa sasa watu wanalenga michezo ya Olimpiki.
Siku ya Alhamisi, Korea Kaskazini ilisema kuwa haina mpango wa kukutana na maafisa wa Marekani , kulingana na chombo cha habari nchini Korea Kaskazini KCNA.
Serikali ya Korea Kusini imesema kuwa mwezi uliopita kwamba wanajeshi 13,000 na vifaa 200 vilipatikana karibu na uwanja wa ndege wa Pyongyang katika kile kinachoonekana kuwa gwaride la majaribio.
Wataalam wanasema Korea Kaskazini inatarajiwa kuonyesha silaha zake za masafa marefu.
Image captionNi Silaha gani ambazo Korea Kaskazini inamiliki
''Kile tunachotarajiwa kuona katika gwaride hilo la kijeshi ni magari ya kubeba silaha, idadi yake na iwapo yanabeba silaha mpya'' , alisema David Schmerler, mchanganuzi wa Korea Kaskazini katika kituo cha James Martin cha masomo ya kuzuia kusambaa kwa silaha.
Mahakama ya kijeshi nchini Somalia, imemhukumu
mtu mmoja adhabu ya kifo kwa kutekeleza shambulio mbaya zaidi nchini humo,
mwezi Oktoba mwaka uliopita.
Hassana Adan Isaq alishutumiwa kwa kuongoza
kundi dogo la al-Shabaab liliotekeleze shambulio hilo.
Wakati kesi ilipokuwa inasikilizwa , kijana huyo
wa miaka 23 alikataa uhusiano na tukio hilo.
Watu wengine wawili wamepatikana na hatia kwenye
kesi hiyo na kupewa adhabu ndogo.
Lori moja lililokuwa limejazwa vilipuzi,
lililipuka nje ya hoteli moja mjini Mogadishu Oktoba mwaka jana wa 2017 na
kusababisha vifo vya zaidi ya watu 500.
Taarifa katika vyombo vya habari vya kimataifa leo February 7, 2018 ni kuhusiana na tukio lililotokea katika mji wa Hualien nchi Taiwan ambapo majengo marefu yameporomoka na kusababisha vifo vya watu wawili na wengine zaidi ya 200 wakijeruhiwa huku 150 wakiwa wamepotea.
Majengo hayo yameporomoka baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi katika mji huo lenye kipimo cha 6.4 lililoupiga mji huo wa kitalii usiku wa kuamkia Jumatano ya leo.
Inaelezwa kuwa watu wengi waliokuwa ndani ya majengo hayo bado wamenasa humo na juhudi za kuwanasua zinaendelea. Mji huo unakadiriwa kuwa na wakazi takribani 100,000.
Rais Jacob Zuma atajiuzulu mara tu baada ya kukamilisha orodha ya masharti yake katika mpango uliofikiwa Jumanne kati yake na kiongozi mkuu wa ANC Cyril Ramaphosa kisha kuthibitishwa na vyanzo Jumanne usiku.
Makubaliano hayo ndiyo yaliyosababisha kuahirishwa kwa mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa chama tawala cha African National Congress (ANC) uliopangwa kufanyika Jumatano ili kulazimisha Zuma kuondoka ofisini.
Mkutano huo ulikuwa umepangwa kufanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Mount Nelson mjini Cape Town na ungepokea mapendekezo kutoka Kamati Kuu ya Taifa ya ANC kwamba Zuma aondolewe kama mkuu wa nchi.
Mkutano kati ya Zuma na Ramaphosa ulifanyika baada ya Spika wa Bunge, Baleka Mbete kutangaza kuahirishwa kwa hotuba ya kitaifa iliyokuwa itolewe na Zuma Alhamisi.
Zuma alitumia Jumanne asubuhi akifanya vikao na kamati za Baraza la Mawaziri mjini Tuynhuys. Baadaye, alikwenda Genadendal yaliko makazi yake ya kifahari huko Cape Town ambako alikutana na Ramaphosa baada ya saa 10:00 jioni pamoja na Katibu Mkuu wa ANC, Ace Magashule.
Januari 6, 2018, Mbete alitangaza kuahirishwa kwa muda usiojulikana kwa hotuba ya hali ya nchi maarufu kama Sona iliyokuwa itolewe na Zuma.
Jumanne jioni, Magashule aliiambia TimesLIVE kuwa mkutano kati ya marais wawili ulikuwa "wa kujenga na wenye mafanikio".
"Nilikuwa huko ... niliwaacha marais wawili hao kujadili mambo yao mimi nilirudi kuungana nao mwishoni," alisema.
Magashule alisema Zuma na Ramaphosa walikubaliana kuwa uamuzi wa kuahirishwa hotuba ya rais ulikuwa sahihi.
"Walikubaliana pia kuwa mkutano wa dharura wa NEC ulioitishwa unapaswa kuahirishwa baada ya majadiliano yao yenye kujenga," alisema.
Magashule hakutaka kuthibitisha ikiwa Zuma amekubali kujiuzulu, ingawa viongozi wengine wa ANC walidokeza kuwa mpango uliokubaliwa utamwezesha Zuma "kuondoka kwa njia ya heshima".
Hata hivyo alidokeza kwamba majadiliano kati ya Ramaphosa na Zuma yaliridhia haja kubwa ya NEC kujadili kuondoka kwake.
Katibu mkuu huyo hakuweza kusema nani atatoa hotuba mara tarehe mpya itakapotangazwa.
Israeil yatoa ilani kwa maelfu ya wahamiaji wa kiafrika ikiwataka
waondoke kufikia mwezi Machi. Maafisa wanasema kwamba endapo onyo hilo
halitotekelezwa wahamiaji huenda wakajikuta wakikamatwa na kufungwa
jela.
Israel imeanza kutoa onyo kwa maelfu ya wahamiaji wa kiafrika tangu hapo jana ikiwataka waondoke nchini humo kufikia mwezi Machi. Maafisa wanasema kwamba endapo onyo hilo halitotekelezwa wahamiaji huenda wakajikuta wakikamatwa na kufungwa jela.
Maafisa nchini Israeli wameshaanza hatua ya kugawa vikaratasi vya ilani kwa wahamiaji wa kiafrika kuanzia hapo jana wakitakiwa kufunganya virago kwa khiari na kuiaga nchi hiyo chini ya mpango maalum unaolenga kuwaondowa kiasi watu 38 elfu wanaoomba hifadhi katika taifa hilo la Mashariki ya Kati, amesema msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Israel.
Ilani hiyo inayotowa muda wa miezi miwili kwa wahamiaji kuondoka inatajwa kwamba inatolewa kwa wanaume wasiokuwa na watoto. Serikali ya Israel inawataja waomba hifadhi walioko nchi humo kuwa ni wahamiaji wanaotafuta maslahi ya kiuchumi ikiwaita kwamba ni watu waliojipenyeza nchini humo.
Hivi karibuni waziri mkuu Netanyahu alisikika akisema:
''Watu waliojipenyeza kinyume cha sheria nchini wana chaguo rahisi-ama kutoa ushirikiano na sisi na kuondoka kwa khiari,kwa heshima na kihalali au tutalazimika kutumia njia nyingi zilizoko kwenye uwezo wetu,na ambazo pia ziko kisheria.Nataraji kwamba wataamua kushirikiana nasi.''
Kwa mujibu wa mpango wa Israel wahamiaji watakaoamua kuchagua kuondoka kwa khiari watapewa dolla 3,500 pamoja na tiketi ya ndege ya kwenda nchi nyingine ambayo haikutajwa. Wanawake ,watoto na kina baba wanaotegemewa na watoto wao hawaguswi katika mpango huo. Hata hivyo kuanzia mwezi Aprili kiwango cha dolla 3500 zinazotolewa kitapunguzwa taratibu na endapo kuna mhamiaji aliyeamua kubakia katika nchi hiyo atakuwa katika uwezekano wa kufungwa jela.Wengi wa wakimbizi wanasema wanakhiari kufungwa kuliko kurudishwa barani Afrika. Uamuzi wa Isreal umekosolewa na mashirika mbali mbali ya kutetea haki za binadamu.
Tamara Newman, mkurugenzi wa mahusiano ya kimataifa katika kitengo maalum kinachowashughulikia wakimbizi na wahamiaji Israel anasema:
''Mpango wa Israel wa kuwaondoa waomba hifadhi 38,0000 kuwapeleka Rwanda pasipo khiari yao ni kitu kisichokubalika kabisa katika nchi yenye demokrasia ambayo imetia saini makubaliano ya kimataifa kuhusu wakimbizi. Serikali inawaambia wahamiaji sasa kwamba wana njia mbili za kuchagua ama kupelekwa Rwanda au kutiwa jela kwa kipindi kisichojulikana. Hili sio chaguo la kweli.tafiti zote zimetuonesha kwamba wote waliopelekwa Rwanda maisha yao yamezidi kuwa hatarini''
Wengi wa watu wanaoomba hifadhi nchini Israel wanaokabiliwa na hali hiyo ya kuondolewa kwa nguvu ni raia wa Sudan na Eretrea. Kadhalika Uganda na Rwanda zinatajwa kwamba ni nchi ambazo wakimbizi hao huenda wakapelekwa ingawa nchi hizo zimekanusha kuwa ni vituo vya kuwapokea wahamiaji watakaorudishwa Afrika kutoka Israel.