DAR ES SALAAM
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli amesema
uzinduzi wa hati ya kusafiria ya kierektroniki utamaliza changamoto za
usafiri nnje ya nchi ikiwemo biashara haramu za madawa ya kulevya.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na wageni wengine ambao ni Makamu wa rais wa
Tanzania Mama Samiah Suluh, Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk Mohamed Shein na
viongozi wengine wa Serikali.
Aidha ameelezea kuwa uwajibikaji wa serikali awamu ya tano ni chachu ya maendeleo hayo yaliyofikiwa katika kuimarisha uchumi wa Tanzania kwa kuangazia utatuzi wa vikwazo vya kibiashara nnje ya Tanzania.
Katika hatua nyingine ameitaka idara ya Uhamiaji kujitathimini katika
utendaji wake akitolea mfano wa ukamatwaji wa mamia ya wahamiaji haramu nchini
katika mikoa ya Mbeya na Iringa .
Hati ya kusafiria ya kierektoniki itapatikana kwa kiasi cha shiringi
laki moja na nusu.
Chanzo:Tbc
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment