NSIMBO
Soko la Katumba Mnyaki linalomilikiwa
na halamshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi halina choo tangu kuanzishwa
kwake hali inayosababisha baadhi ya wafanyabishara
kujisaidia vichakani ambopo muda wowote huenda mlipuko wa ugonjwa wa
kipindupindu ukatokea.
Hayo yamebainishwa na wakazi wa Kata
ya Katumba wanaotumia soko hilo ambapo wamesema wanaishi kwa taharuki ya
kukumbwa na kipindupindu kutokana na kukithiri kwa uchafu na ukosefu wa choo
katika soko hilo.
Kwa upande wao mwenyekiti wa soko
hilo Bw.Leonard Kigwasu na Afisa Mtendaji wa vijiji vya Mnyaki A na B Bw.Kombo
Masatu wamekiri kuwepo kwa uchafu sokoni hapo huku wakisema choo kinatarajiwa
kukamilika katika kipindi cha miezi miwili ijayo.
Baadhi ya wamiliki wa maduka ya
kibiashara wamesema wanatozwa kuanzia shilingi elfu sita na mia tano huku
wafanyabishara wanaouzia bidhaa chini wakilipa ushuru kila wanapouza.
Kwa mjibu wa takwimu iliyotolewa hivi
karibuni na Diwani wa Kata ya Katumba Senetor Braka,jumla ya vijiji 16 vya kata
hiyo vyenye jumla ya wakazi zaidi ya elfu hamsini wanapata huduma ya soko hilo.
Source: Issack Gerald
No comments:
Post a Comment