Mwandishi wetu Mdaki Hussein akiwa na wanachi wa kiji cha kibunga
|
Zaidi ya wakazi 1000
wa kijiji cha Kabuga katika kata ya Kanoge halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi
wanakabiliwa na adha ya maji safi na salama.
Baadhi ya Wanawake katika eneo hilo walipozungumza na Mpanda
radio fm wamewalaumu viongozi wa kijiji hicho kutokana na kushindwa kutatua
tatizo na wengine wamesikika walisema walipewa ahadi hewa.
mwandisha wetu Alinanuswe Edward akifanya mahojiano na mwananchi wa kijiji cha kabunga |
Miongoni mwao wameeleza kuwa utawala wa serikali ya kijiji hicho, umeingiza udanganyifu hata katika mambo ya msingi kama vile huduma za kijamii.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Benjamini Ezekiel amekili kuwepo
kwa tatizo hilo na kueleza jitihada za serikali kuwa ni kuongeza idadi ya
vizima ili viweze kukidhi mahitaji ya wakazi.
Mwandisha wetu Alinanuswe Edward akifanya mahojiano na mwananchi wa kijiji cha kabunga |
Kijiji hicho kilicho kaskazini mwa mkoa wa Katavi ulio kusini magharibi ya Tanzania kina kisima kimoja tu, jambo ambalo wenyeji hasa wanawake wanadai kutumia muda mwingi kutafuta maji kuliko kufanya kazi za kimaendeleo.
@habari na alinanuswe Edward.
No comments:
Post a Comment