MPANDA
Jamii mkoani katavi imetakiwa kuwajali watu
walio katika mahitaji maalumu ili kuwawezesha makundi kushiriki katika shughuli
mbalimbali za uzalishaji mali
Afisa ustawi wa jamii wa Manispaa ya Mpanda Bi
Agness Buraganya ameiambia mpanda radio mapema leo kuwa idara ya ustawi wa
jamii inaendelea kutoa elimu shirikishi ili kuhakikisha jamii inapata uelewa wa
kuishi na watu walio katika makundi hayo
Katika hatua nyingi Bi Buraganya amesma endapo
jamii inakuwa na mwamko wa kuwatambua watu walio kwenye makundi hayo serikali
mkoani hapa iko tayari kuyaunganisha na fursa mbalimbali zitakazowawezesha
kuijtegemea
Amesema kwa mwaka wa 2018 usatawi wa jamii
mkoani hapa imejipanga kushughulikia masuala mbalimbali ikiwemo kupunguza
ongezeko la mimba za utotoni.
Chanzo: Haruna Juma
No comments:
Post a Comment