KATAVI
Shule ya msingi Misunkumilo iliyopo Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya madarasa na madawati hali inayopelekea kushuka kwa kiwango cha elimu na ufaulu kwa ujumla
Geofrey Kisaye ni mwalimu mkuu msaidizi wa shule hiyo amekili kuwepo kwa tatizo hilo huku akilitaja kuwa kikwazo katika mstakabali wa maendeleo ya taaluma.
Wanafunzi wa shule hiyo hawakusita kuiomba serikali kuongeza vyumba vya madarasa pamoja na madawati ili kuepukana na msongamano wa wanafunzi darasani.
Naye afisa elimu taaluma wa shule za msingi Manispaa ya Mpanda Rashid pili amesema serikali inaendelea na mkakati wa uimarishaji wa miundo mbinu katika shule mbali mbali.
Tangu kuanzishwa kwa sera ya elimu bure nchini na kutekelezwa mwaka 2016 kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya wanafunzi.
Chanzo:Isack Gerald
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment