Rais wa Marekani Donald Trump |
Rais Donald Trump wa Marekani ametangaza mkakati mpya wa kijeshi
kuhusu Afghanistan na eneo la Asia ya Kusini, unaorudi nyumba katika kulijenga
taifa hilo na badala yake kipaumbele kitakuwa kuwasaka na kuwaua magaidi.
Mkakati
huo mpya umetangazwa katika wakati ambapo wanamgambo wa kundi la Taliban
wanaongeza mashambulizi yao katika wilaya za maeneo kadhaa ya nchi, na huku
Marekani ikiwa inaelekea kutimiza miaka 17 ya kuwepo kijeshi nchini Afganistan.
Trump
amesema malengo makuu ya mkakati huo ni kuliharibu kundi linalojiita Dola la
Kiislam IS, kulisagasaga kundi la al-Qaeda na kulizuia kundi la Taliban
kuidhiti Afghanistan.
"Hatujengi
tena taifa. Tunawaua magaidi. Hatua inayofuata ya mkakati wetu mpya ni kubadili
mbinu na jinsi ya kukabiliana na Pakistan. Hatuwezi tena kukaa kimya kuhusu
namna Pakistan inavyoyapa usalama mashirika ya kigaidi, Taliban, na
makundi mengine ambayo yamekuwa tishio kwa kanda nzima na zaidi ya hapo. Pakistan
itafaidika kwa kushirikiana na jitihada za Marekani huko nchini
Afghanistan," amesema rais wa Marekani, Donald Trump.
Muda
mchache baada ya hotuba hiyo ya Trump iliyorushwa katika televisheni akiwa
mbele ya wanajeshi wa kambi ya Fort Myer kaunti ya Arlington, huko Virginia,
kundi la Talibal lilitoa tamko la kuendeleza mapigano hadi pumzi yao ya mwisho
na kuonya iwapo Marekani haitaondoka Afghanistan basi nchi hiyo itageuka kuwa
eneo la makaburi ya wanajeshi wa Kimarekani.
Wanajeshi wa Kimarekani
wakipandisha bendera ya Marekani, jimbo la Helmand Afghanistan
Afghanistan
hata hivyo imeipokea hotuba ya Trump kwa mitazamo tafauti. Baadhi ya raia wa
kawaida wamefurahia maneno makali ya Rais Donald Trump dhidi ya Pakistan
alipoishutumu nchi hiyo kwa kuwahifadhi magaidi huku wakiwaua wanajeshi wa
Kimarekani katika nchi jirani ya Afganistan.
Lakini
wachambuzi wa Pakistan wanaonya kutengwa kwa nchi hiyo kama mkosa pekee
kutasababisha kuongezeka kwa ushawishi wa nchi kama Urusi, China na hata Iran
nchini humo.
Waafghani
wengi waliohojiwa na shirika la habari la AP katika mji mkuu wa Kabul,
wameelezea hofu zao juu ya hali kuwa mbaya zaidi nchini, wakisikitikia
rushwa, kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira na mauwaji mabaya
yanayotokana na mashambulizi.
Kwa upande wa nchi za magharibi, Uingereza leo imekubaliana na
uamuzi wa Rais Trump wa kuongeza kasi katika kampeni ya kijeshi dhidi ya waasi
wa kundi la Taliban nchini Afghanista.
Uingereza na washirika wengine wa nchi za Ulaya wameahidi kutoa
wanajeshi zaidi kulisaidia jeshi la Afghanistan mwezi Juni, huku Waziri wa
Ulinzi wa Marekani Jim Mattis akisema kwa wakati huo kwamba idadi ya wanjeshi
nchini humo ilikuwa ikipungua haraka mno.
Kwa sasa Marekani ina wanajeshi wapatao 8,500 nchini Afghanistan
wanaopigana vita ambavyo Marekani ilijitumbukiza ndani yale baada ya mashambulizi
ya kigaidi ya Septemba 11, mwaka 2001
No comments:
Post a Comment