DODOMA
Serikali
imesema inatarajia kujenga miundombinu ya maji katika ziwa Tanganyika ili
kuweza kuboresha huduma ya maji safi na salama katika mkoa wa katavi
Hayo
yamesemwa leo bungeni na waziri wa maji na umwagiliaji mhandisi Isack Kamwela wakati akijibu swali la mbunge wa
viti maalum (CHADEMA) Rhioda Kunchela
aliyetaka kujua utayari wa serikali kutumia vyanzo vya maji viliyopo mkoani
katavi kutatua kero ya maji kwa wananchi wake
Akijibu
swali hilo Mhandisi Kamwela amesema serikali kupitia wizara ya maji
imeshatekeleza miradi kadhaa na inaendelea kutatua kero ya maji katika mkoa wa
katavi na wilaya zake
Kauli
hiyo ya serikali inakuja huku kukiwa na idadi kubwa ya wakazi wa mkoa wa katavi
wanaotumia maji kutoka vyanzo visivyo rasmi kwa matumizi mbalimbali
Chanzo:TBC1
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment