Wednesday, 24 January 2018

Jeshi la zimamoto na Uokoji mkoani katavi limekiri kushindwa kutoa miili hiyo kwa madai ya ukosefu wa vifaa kazi vinavyowezesha kurahisisha uokoaji huo.


MPANDA
Miili ya vijana wawili waliofunikwa na kifusi cha udongo katika machimbo ya dhahabu yaliyo kijiji cha Ibindi  Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi bado haijaopolewa kwa wiki ya pili sasa.
Mpanda radio imefika katika eneo la Kwa Songoro lililopo kijiji cha Ibindi na kuzungumza na baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo ambao wameelea kusikitishwa na tukio hilo.
Kwa mujibu wa mashahidi wameiambia  Mpanda radio kuwa mmoja ya vijana waliopoteza maisha Azam Lawrence Nyembeke mkazi wa Iringa  ndugu zake hawana taarifa mpaka sasa.
Licha ya juhudi mbalimbali zilizofanywa na wachimbaji wakishirikiana na wananchi wa eneo hilo Jeshi la zimamoto na Uokoji mkoani katavi limekiri kushindwa kutoa miili hiyo kwa madai ya   ukosefu wa vifaa kazi vinavyowezesha kurahisisha uokoaji huo.

Uchimbaji wa madini ni moja kati ya shughuli ianyowakusanya vijana kutoka mikoa mbali nchini lakini wakiwa katika hatari kubwa ya kupoteza maisha kutokana na teknolojia duni ya uchimbaji.
Chanzo: Haruna Juma 
#Changia Damu Okoa Taifa

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...