MPANDA
Kata ya Magamba
wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi inakabiliwa na ukosefu wa huduma ya umeme hali
inayosababisha huduma duni katika vijiji hivyo.
Akizungumza na Mpanda Radio diwani wa Kata hiyo Mh.Philipo Kalyalya amesema suala la ukosefu wa umeme katika kata hiyo limekuwa na changamoto kubwa hali inayopelekea kukwamisha huduma mbali mbali za kijamii
Kwa upande wake Meneja uhusiano wa tanesco mkoani hapa Bw. Amon Michael amewataka wakazi katika maeneo hayo kwenda katika ofisi za Tanesco kujiandikisha kwa ajili yakufungiwa umeme kabla bei hazijabadilika.
Kata ya Magamba
ni miongoni mwa kata zilizopitiwa na mradi wa rea ya awamu ya tatu baadhi ya
maeneo mpaka sasa kutajwa kukosa huduma ya umeme.
Chanzo:Neema Manyama
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment