Wananchi wa kijiji cha Ilalangulu kata
ya Kibaoni katika Halmashauri ya Wilaya Mpimbwe Mkoani Katavi wameiomba
serikali kuwaboreshea huduma ya maji ili kuondoa adha wanayoipata katika kijiji
hicho.
Wamesema hayo wakati wakizungumza na
Mpanda radio na kusema kuwa maji yaliyopo hayakidhi mahitaji ya kijiji hicho
kutokana na ukubwa na wingi wa wakazi kijijini hapo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji
hicho amesema kuwa tatizo la maji katika kijiji chake ni kubwa na tayari
halmashauri imeshapata taarifa hiyo na imeanza kuifanyia kazi.
Hata hivyo Kaimu mtendaji wa kijiji
hicho Samweli Makobo amesema kuwa serikali iangalie ukubwa wa kijiji na kwa
wananchi waliopo pembezoni mwa kijiji ili kukidhi mahitaji ya wanakijiji wote
hasa wafugaji.
Maji ni muhimu kwa maisha ya binadamu
hivyo serikali inatakiwa kutatua changamoto hiyo hasa kwa maeneo ya vijijini
ambayo ndiyo yenye changamoto kubwa ya upatikananji wa maji.
Chanzo:Furaha Kimondo
No comments:
Post a Comment