Na;Ezelina Yuda
Mtoto
mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai
kandokando ya uwanja wa azimio manispaa
ya Mpanda Mkoani Katavi na mwanamke ambaye hajafahamika majina wala makazi
yake.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo,wamebainisha kuwa Kichanga hicho ambacho kinasadikiwa kimetupwa tangu majira ya jioni kimeokotwa majira ya saa kumi alasiri.
Wakizungumza na Mapanda Fm , mashuhuda hao wamesikitishwa na kitendo hicho huku wakiomba hatua kali zichukuliwe dhidi ya mwanamke atakayebainika kutenda unyama huo.

Afisa Ustawi wa jamii manispaa Redgunda Mayolwa ameiomba
jamii kutoa ushirikiano kwa viongozi wa serikali na jeshi la Polisi ambao
wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo,na kumbaini mwanamke aliyetenda tukio hilo
la kinyama na kusema kwamba kitendo cha kutupa mtoto hakina tija kwa
jamii.
Jamii imeshauriwa kutoa ushirikiano kwa viongozi wa ngazi zote ikiwemo Jeshi la
Polisi Ili kuweza kuyakomesha matukio hayo
No comments:
Post a Comment