DAR
ES SALAAM
Chama
cha Chadema,ambacho pamoja na vyama
vingine vitano vilisusia uchaguzi mdogo katika majimbo matatu, sasa ipo
njiapanda kusimamisha wagombea katika majimbo ya Kinondoni na Siha.
Wakati
bado hakijatangaza kubadili msimamo huo, uongozi wa ngazi ya Wilaya ya
Kinondoni umeanza kutoa fomu kwa ajili ya mchakato wa kupata mgombea kwa
maelezo kuwa umeruhusiwa na uongozi wa juu wa chama hicho kikuu cha upinzani.
Lakini
uongozi huo wa juu umesema bado haujafanya uamuzi kuhusu kushiriki uchaguzi
katika majimbo hayo uliopangwa kufanyika Februari 17 na msimamo huo unaweza
kutolewa wakati wowote.
Mkurugenzi
wa Mambo ya Nje na Itifaki wa Chadema, John Mrema amesema jana kuwa wameunda
kamati ndogo inayofanya utafiti kuhusu mchakato huo na kwamba uchukuaji fomu bado haujapewa baraka za ngazi za juu.
Majimbo
hayo mawili yanarudia uchaguzi baada ya waliokuwa wanayashikilia Maulid Mtulia
(CUF, Kinondoni) na Dk Godwin Mollel (Chadema, Siha), kujiuzulu nafasi zao kwa
nyakati tofauti na kuhamia CCM mwezi uliopita.
Source Mwananchi
No comments:
Post a Comment