Rais wa marekani Donald Trump |
WASHNGTON
DC
Rais
Trump hajaonyesha dalili zozote za matatizo ya kiakili kufuatia uchunguzi wa
kiafya na yuko la afya nzuri, daktari wa White House amesema.
Wiki iliyopita Trump
amefanyiwa uchunguzi wa afya wa saa tatu, ambao ni wake wa kwanza tangu awe
rais wa Marekani.
Akiongea na waandishi wa
habari wakati wa mkutano huko White House, Dkt Jackson amesema kuwa kwa jumla
afya ya rais ni nzuri.
Siku ya Ijumaa rais
amechunguzwa na madaktari wa kijeshi katika kituoa cha afya cha Walter Reed
huko Bethesda, Maryland katika uchunguzi uliotajwa kuwa wenye ufanisi mkubwa.
Michael Wolf ambaye ni mwandishi wa kitabu cha
Fire and Fury: Inside the Trump White House, ni kuwa wafanyakazi wote wa White
House walimuona Trump kama mtoto.
Chanzo:Dw swahili
No comments:
Post a Comment