Wafanyabiashara wa soko
la Mpanda Hoteli lililoko Halmashauli ya Manispaa ya Mpanda wameiomba serikali
kuwaboreshea miundo mbinu ya soko hilo kama walivyoahidiwa na mkurugenzi wa
manispaa hiyo.
Wameyasema hayo
walipozungumza na Mpanda Radio na kusema kuwa kuchelewa kwa uboreshwaji wa soko
hilo kunaathiri biashara zao hasa katika kipindi cha mvua na huku wanalipia
tozo .
Mwenyekiti wa soko hilo
Boniface Mganyasi amesema kuwa yapata miezi mitatu serikali iliahidi
kuwaboreshea soko hilo lakini mpaka sasa hawajapata mrejesho wowote.
Uboreshaji wa masoko ni
mpango mkakati uliopo katika halmashauri ya Manspaa ya Mpanda kwaajili ya
kuhahakisha masoko hayo yanakua na mazingira bora kwa wafanyabiashara.
Chanzo:Furaha Kimondo
No comments:
Post a Comment