Mwenge wa Uhuru wilayani Tanganyika umezindua miradi
14 yenye thamani ya shilingi bilioni nne
laki sita hamsini na nne elfu na senti
hamsini.
Akizindua miradi hiyo kiongozi wa mbio za mwenge
kitaifa mwaka huu Charles Francis Kabeho
amesema wananchi wanatakiwa kutumia miradi hiyo katika kukuza uchumi na kulinda
raslimali za nchi.
Baadhi ya Miradi iliyozinduliwa ni mradi wa kiwanda cha kufyatua matofali kata
ya Majalila, mradi wa EP4R wa bweni la sekondari Kabungu na
kampeni ya kuziua na kupambana na rushwa shule ya msingi Mpembe kata ya
Sibwesa.
Mwenge wa uhuru unaendelea kukimbizwa katika maeneo mbalimbali mkoani Katavi ambapo kwa siku ya leo umekamilisha mbio zake waliyani Tanganyika .
Chanzo:Ezelina Yuda
No comments:
Post a Comment