Thursday, 14 September 2017

Wakazi wa mtaa wa Mpadeko katika kata ya Makanyagio wamelaumu uongozi wa mtaa huo kutokana na kushindwa kudhibiti vitendo vya wizi katika eneo lao.

MPANDA
Wakazi wa mtaa wa Mpadeko katika kata ya Makanyagio Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda wamelaumu uongozi wa mtaa huo kutokana na kushindwa kudhibiti vitendo vya wizi katika eneo hilo.
Wakizungumza na Mpanda radio wamesema wizi wa mifugo pamoja na bidhaa mbali mbali za majumbuni umeshika kasi kila kuitwapo leo lakini hawaoni hatua zinazo chukuliwa ili kupambana na hali hiyo.
Kwa upande wa  mwenyekiti wa mtaa  wa Mpadeko Benard Nkana wakati amekili   kupokea malalamiko hayo na kuahidi kuchukua hatua za kisheria kwa wale wote wanaohusika na vitendo hivyo.

Mara kwa mara vitendo hivyo vimeripotiwa na wakazi hao ambapo awali wizi huo ulieneo katika kata nzima ya Makanyagio

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...