Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam |
Pia inadaiwa alikuwa ni mmoja wahusika wa matukio mbalimbali ya kijambazi ikiwemo kuvamia mabenki na kuua askari wanane wa wilaya ya Kibiti. Kapela pia anadaiwa kuhusika na mauaji ya Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Newala mwaka 2013, uvamizi wa kituo cha polisi Stakishari mwaka 2015, kuuwa askari watatu na kupora silaha mbili aina ya SMG kwenye benki ya CRDB Mbande mwaka 2016, na pia kuvamia benki ya Access Mbagala pamoja na benki ya NMB Mkuranga.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu, Lazaro Mambosasa alisema tukio hilo lilitokea Septemba 12 maeneo ya Kivule Chanika.
“Mtuhumiwa huyu ndiye aliyekuwa kiongozi na mratibu mkuu wa matukio hayo Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani na ametaja wahusika alioshirikiana nao katika matukio yaliyotajwa, hivyo ufuatiliaji bado unaendelea,” alisema Mambosasa.
Alisema kabla ya tukio hilo askari walipokea taarifa ya kuwepo kwa mtu huyo maeneo hayo na kuweka mtego na kufanikiwa kumkamata mtu huyo baada ya kumjeruhi kwa risasi ya goti la mguu wa kulia na mkono wa kushoto wakati akijaribu kukimbia.
Aliongeza kuwa jambazi hilo lilifika maeneo hayo ya Kivule kwa ajili ya kuuguza majeraha ya risasi aliyopigwa ambapo alikuwa anatibiwa na bibi mmoja baada ya kukimbia operesheni ya Kibiti.
“Askari wetu waliweka mtego muda wa saa nne usiku na kuzingira nyumba aliyokuwa akipatiwa matibabu, lakini badala yake alitokea nyumba nyingine alipoona askari alianza kukimbia ndipo alipigwa risasi kwenye goti la kulia, begani chini ya mkono wa kushoto,” alisema Mambosasa.
Mambosasa alisema baada ya upekuzi mtuhumiwa huyo aligundulika kuwa na makovu makubwa matatu ya risasi sehemu mbalimbali ikiwemo shavu la kulia, bega la kulia na mguu na ndiyo alikuwa akipata matibabu hayo.
@habari na habari leo
No comments:
Post a Comment