Friday, 16 February 2018

Wakazi wa kijiji cha Manga katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wameiomba serikali kuwaongezea mabomba ya maji ili kuendana na idadi ya wananchi waliopo katika kijiji hicho.



MPANDA

Wakazi wa kijiji cha Manga katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wameiomba serikali kuwaongezea mabomba ya maji ili kuendana na idadi ya wananchi waliopo katika kijiji hicho.

Wakizungumza na Mpanda Radio kwa Nyakati tofauti,wakazi hao wamesema kwa sasa wanapoteza muda mwingi kusubiri maji na hivyo kuchelewa kufanya shughuli nyingine za maendeleo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Manga Bw.Mathias Nswima amesema kijiji hicho chenye zaidi ya wakazi elfu tatu na mia nane,kina visima vitatu huku vingine vikiwa vimeharibika na kukosa matengenezo kwa madai kuwa vipuli havipo kwa sasa.

Kwa mjibu wa serikali ya awamu ya tano ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ni kuwa maeneo yote nchini yanatarjiwa kuwa na maji kwa asilimia 95 ifikapo mwaka 2020.

 Chanzo: Issack Gerald


No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...