Kibao cha shule ya msingi nsanda iliyopo katumba B |
Shule ya msingi nsanda iliyopo kata ya kanoge
halmashauri ya nsimbo mkoan katavi madarasa yake yabaki bila wanafunzi
shule ya nsanda iliyojengwa kwa hisani ya Serikali ya watu wa
Uingereza pamoja na shirika la Wakimbizi UNHCR, kwa usimamizi wa Serikali ya
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania sasa madarasa haya yaliyojengwa kisasa
yanabakia kuwa magofu!
tunaenda wapi jamani,amesema Paulo Johnson katika
mahojiano huku akibubujikwa na machozi.
Safari yangu imeanzia katika shule ya Msingi Nsanda
iliyopo Kasikazini mwa mkoa wa Katavi ulio kusini magharibi mwa Tanzania.
choo cha kisasa kilichopo shuleni nsanda |
Makazi ya wananchi katika
eneo hili yameharibiwa kabisa kwa kuchomwa moto na mamlaka ya misitu kwa kile
kinachodaiwa kuwa ni sehemu ya hifadhi ya misitu.
kilomita tano kutoka katika eneo hilo nimeshuhudia
mamia ya wakazi wakiwa wameweka kambi chini ya miti pamoja na familia zao.
Mama moja amesema hali ni mbaya anahofia kuwapoteza
watoto wake kutokana na magonjwa.
Kwa upande wa mkuu wa wilaya ya
Mpanda ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Bi
Lilian Matinga mapema mwanzoni mwa mwezi agost alikili kuwaondoa wakazi katika
maeneo hayo kwa kile alichokiita kuwa wamevamia maeneo hayo na kwamba ni hatari
katika ustawi wa mazingira.
@habari na mwandishi wetu Alinanuswe Edward
@habari na mwandishi wetu Alinanuswe Edward
No comments:
Post a Comment