Umoja
wa Waendesha Pikipiki maarufu kama Boda boda Katika Manispaa ya Mpanda Mkoa wa
Katavi umewataka baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitumia jina
la kazi yao kufanya vitendo vya Uhalifu kuacha tabia hiyo mara moja.
Wamebainisha
hayo wakati wakizungumnza na Mpanda Redio wamesema kuna baadhi ya watu wamekuwa
na tabia ya kutumia jina la boda boda kufanya vitendo vya uhalifu hususani wizi
ukabaji hali ambayo huleta taswila mbaya katika kazi yao
Aidha
wametoa ushauri kwa wateja wao kuwa na namba za simu kutoka katika vituo vya
boda boda vinavyo tambulika ili kuepusha matatizo kama hayo ya wizi kwa wateja
ambayo yamekuwa yakifanywa na watu ambao sio wema
Katika
hatua nyingine wamelishukuru Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani
kuanzisha mfumo wa kuwepo kwa vituo maalumu vya kufanyia kazi zao hali ambayo
imerahisisha utendaji wa kazi nakupunguza usumbufu ambao ulikuwa unajitokeza
hapo awali.
Chanzo:Paul Mathius
No comments:
Post a Comment