Imeandikwa na. Prosper Kwigize, Kasulu, Kigoma
Sisi vijana wenye vipaji tupo wengi sana vijijini, elimu yetu ni ya darasa la saba lakini vipaji vyetu ni zaidi ya aliyesoma hadi chuo kikuu, tunachangia pato la Taifa kupitia kazi za mikon.
Bahati mbaya thamani yetu kwa jamii ni ndogo, wanaothaminiwa ni walioajiriwa serikalini ambao wengine hata hatuoni tija ya usomi wao.Mwaka 2014 serikali ya Tanzania ilitangaza rasmi sera mpya ya elimu nchini humo, ambayo ilitambua elimu ya vipaji maalumu vya kisayansi kama njia muhimu ya kukuza uchumi katika dunia ya utandawazi
Ni kwa sababu ya masomo ya teknolojia ya habari na mawasiliano maarufu kama TEHAMA pamoja na stadi za kazi yalihimizwa kufundishwa katika ngazi za elimu ya msingi, sekondari na vyuo ili kuwaandaa vijana kuwa na uwezo wa kuingia katika ushindani wa soko la ajira duniani.
Mwandishi Prosper Kwigize, Kigoma, Tanzania Katika mahojiano ya DW na Waziri wa Elimu nchini Tanzania Profesa Joyce Ndalichako katika kipindi cha Kinaga ubaga cha mwezi Octoba 2014, katika moja ya majibu yake juu ya kuibua vipaji alisema serikali imeandaa utaratibu wa kupita nchi nzima kuwatambua vijana na watoto wenye vipaji mbalimbali.
Hata hivyo kwa kijana Salumu Rashid kijana mtanzania mwenye umri wa miaka 20 haoni kama serikali ya Tanzania inadhamira thabiti ya kuwasaidia vijana wenye vipaji nje ya mfumo rasmi wa elimu.
Salum amevumbua matumizi ya mabaki ya magurudumu ya magari kwa ajili ya utengenezaji wa majiko ya kutumia nishati ya mkaa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.
Mtaalamu wa Majiko ya Waya Bw. Salum Rashid akionesha majiko yaliyokamilika tayari kwa kwenda sokoni |
Kiwanda chake kidogo kina wafanyakazi sita, ambao hufanya kazi ya kukusanya matairi kutoka katika majalala mbali mbali katika miji ya Kibondo, Kasulu, Kigoma na katika nchi jirani ya Burundi na kisha kuyachoma ili kutoa waya ambazo ndhizo hutumika kutengeneza majiko hayo
Jumla ya majiko 10 hadi 40 hutengenezwa kila siku na vijana hawa, ambapo huyauza kwa bei kati ya shilingi 10,000 hadi 20,000 kwa jiko moja, kutokana na idadi inayozalishwa kila siku Bw. Salum hukusanya kiasi cha shilingi 50,000 hadi 120,000.
Kiwanda chake sasa kilichoko katika mazingira duni ya mjini Kasulu, kinafanya kazi kama kituo cha mafunzo kwa vijana kadhaa ambao baada ya kuona tija ya maisha ya mwenzao, nao wamejitokeza kupata mafunzo hayo ya aina yake.
Majiko yanayotumia mkaa kwa kupikia ambayo yametengenezwa kwa kutumia waya za magurudumu ya magari yaliyokwisha muda wake |
Bi. Neema Segeza mwanamke aliyepata mafunzo ya utengenezaji wa majiko |
Wote wawili kwa pamoja wana matarajio ya kununua viwanja na kujenga nyumba kwa ajili ya makazi yao na kutafuta eneo maalumu kwa ajili ya kiwanda cha majiko hayo Hata hivyo chngamoto ya ukosefu wa mitaji na serikali kutotenga ardhi kwa ajili ya viwanda vya ubunifu na usanifu wa kazi za mikono ni kikwazo kwa vijana wengi wenye vipaji nchini Tanzania.
Bw. Salum Rashid na Bi. Neema Segeza wakiwa katika shughuli za utengenezaji wa majiko ya waya mjini Kasulu |
Sera ya Elimu na Mafunzo ufundi Tanzania Kwa mujibu wa sera ya elimu nchini Tanzania ya mwaka 2014, utoaji wa elimu nchini humo unatekekelezwa kama sekta mtambuka ambapo wizara zaidi ya moja huhusika jambo linalotajwa kuwa sababu ya kudhorota kwa usimamizi.
Uchambuzi wa tathmini ya utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995, umeonyesha kuwa matamko 59 kati ya matamko 149 ya Sera hayakutekelezwa.
Kati ya hayo, matamko 25 yalihusu elimu ya msingi na sekondari, 18 yalihusu elimu ya ufundi na 16 yalihusu elimu ya juu.
Tathmini iliyofanywa na wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi ilibaini pia kuwa mpango mkakati wa kuelekeza utekelezaji wa sera hizo haukuandaliwa mpaka mwaka 1997 ulipoanzishwa Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu, na mwaka 2001 ulipoandaliwa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM).
Tathmini ilibaini pia kuwa usimamizi na uendeshaji wa elimu na mafunzo katika ngazi ya mkoa na wilaya unafanywa na mamlaka mbalimbali zinazoongozwa na kanuni na taratibu tofauti pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu jambo linaloibua mkanganyiko wa nani anapaswa kusimamia haswa utoaji wa elimu yenye tija hasa kulingana na soko la ajira.
No comments:
Post a Comment