KATAVI
Wananchi wa wilaya ya
Mpanda mkoani katavi wamelalamikia
shirika la reli kwa kutorekebisha miundombinu ya reli kwa wakati katika eneo la Ugala mpaka Rumbe.
Wakiongea na Mpanda
redio wananchi hao wameeleza kuwa kumekua na ajali nyingi zikitokea kutokana na
miundombinu ya eneo hilo kutokuwa salama kwa usafiri hali inayosababisha
kupotea kwa mizigo.
Mkuu wa kituo cha
reli Mpanda Ndugu Vivian Lyapembile amesema kuwa pamoja na
changamoto wanazopata kwa sasa ila wana ufahamu na tatizo hilo na tayari wameanza mchakato wa
kukarabati eneo hilo.
Hivi karibuni kumekuwa
na changamoto ya usafiri kwa wasafiri wanaotumia usafiri wa treni hali
inayosababishwa na uchakavu wa miundo mbinu kwa baadhi ya maeneo.
Chanzo: Neema Manyama
No comments:
Post a Comment