Monday, 20 November 2017

Meli kubwa ya Jeshi la Jamhuri ya China yenye hospitali (Chinese Hospital Ship) imewasili katika bandari ya Dar es Salaam



 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akitembelea Meli hiyo.

DAR ES SALAAM

Meli kubwa ya Jeshi la Jamhuri ya China yenye hospitali (Chinese Hospital Ship) imewasili katika bandari ya Dar es Salaam ikiwa na madaktari bingwa 381, vifaa na madawa ya kutosha kwa ajili ya kuanza kwa zoezi la upimaji na matibabu bure kwa wakazi wa Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ametembelea Meli hiyo na kujionea namna imesheheni vifaa tiba vya kisasa ambapo ndani yake vipo vyumba 8 vya upasuaji, vyumba vya ICU, wodi za wagonjwa, vyumba vya madaktari, mitambo ya kisasa, maabara na sehemu ya wagonjwa kupumzika.

Tayari Jopo la wataalamu 30 wameenda Hospital za Amana, Temeke, Mwananyamala na Ocean Road kwa ajili ya kukarabati na kufunga vifaa vipya kwa vile vitakavyobainika vilivyoharibika au kufa.

Amesema lengo la serikali ni kuhakikisha hakuna mwananchi anaepoteza maisha kwa kigezo cha kukosa huduma.

Kwa upande wake kiongozi mkuu wa meli hiyo Kamanda Guan Bailinamesema wamekuja na vifaa vya kutosha na madaktari waliobobea hivyo wananchi wajitokeze kwa wingi.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...