Wanajeshi 10 hawajulikani waliko na wengine watano wamejeruhiwa
baada ya manowari ya jeshi la Marekani kugongana na meli ya kubeba mafuta pwani
mwa Singapore, kwa mujibu wa jeshi la wanamaji la Marekani.
Manowari ya USS John MacCain ilikuwa mashariki mwa Singapore
ikijiandaa kutia nanga bandarini wakati iligongana na meli iliyokuwa
ikipeperusha bendera ya Liberia. Shughuli kubwa ya kuwatafuta na kuwaokoa
wanajeshi inaendelea.
Ndicho kisa cha pili kikubwa kinachoikumba meli ya jeshi la
wanamaji wa Marekani miezi ya hivi karibuni.
Ripoti zinasema kuwa manowari hiyo ilikumbwa na uharibifu upande
wake mmoja, lakini jeshi la Marekani lilsema kwa inaelea peke yake kwenda
bandari ya Singapore.
Helikopta za jeshi la Marekani na jeshi la Singapore pamoja na
walinzi wa pwani, wanafanya shughuli za uokoaji. Malaysia nayo imejiunga katika
shughuli hiyo.
Kisa hiki kinatokea siku ya kwanza ya mazoezi ya kila mwaka ya
kijeshi kati ya jeshi la Marekani na Korea Kaskazini, ishara ya ubabe wa
kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini.
USS John Mccain ni moja ya manowari saba za Marekani
zinazoshiriki, lakini kisa hiki kitachangia kuwepo maswali kuhusu shughuli za
jeshi la wanamaji eneo hilo.
Hiki ndicho kikosi kile kile ambacho kilikumbwa na ajali mwezi
Juni, wakati wanajeshi 7 wa Marekania waliuawa. Ni wiki iliyopita tu ambapo maafisa
saba waliadhibiwa kufuatia kisa hicho.
kuwa mkasa wa nne wa kugongana kwa meli za jeshi la Mareknia
mwaka huu pekee.
Kuna taarifa kidogo kuhusu hali ya meli ya mafuta ya Alnic MC na
wahudumu wake.
Meli hiyo ya mafuta inaripotiwa kuwa na uzito mara tatu zaidi na
wa manowari ya jeshi ya USS John McCain, na taarifa zinasema kuwa haikuwa
imebeba mafuta wakati ya ajali hiyo.
Seneta John McCain ambaye jina lake limepewa manowari hiyo, aliandika
kwenye mtandao wa twitter kuwa yeye na mke wake wanawaombea mabaharia hao.
Mwezi Juni mabaharia saba wa Marekani waliuawa wakati manowari
ya USS Fitzgerald iligongana na meli ya mizigo kwenye bahari ya Japan karibu na
bandari ya Yokosuka.
habari kutoka bbc swahili.
No comments:
Post a Comment