Takariban watu 12 wamefariki wakati mashua iliyokuwa imebeba waislamu wa Roningya wanaokimbia ghasia nchini Myanmar ilizama karibu na Bangladesh.
Watu kadha hawajukani waliko baada ya ajali hiyo iliyotokea kwenye mto Naf siku ya Jumapili. Inaamiwa hadi watu 100 wakiwemo watoto walikuwa kwenye mashua hiyo.
Shughuli ya uokoaji kwa sasa inaendelea.
Watu kadha wa jamii ya Rohingya tayari wamefariki wanapojaribu kuvuka kweda nchi jirani ya Bangladesh kutokana na oparesheni ya kijeshi inayoendelea jimbo la Rakhaine.
Idadi kamili ya watu waliokuwa ndani ya mashua haijulikani lakini maafisa wa mpakani nchini Bangladesh wanasema kuwa walikuwa ni kati ya watu 40 hadi 100.
Maafisa wanasema kuwa miili ya watoto 10, mwanamke na mwanamume imepatikana hadi sasa.
Hiki ni kisa cha hivi punde zaidi kinachohusu mashua zinazowasafirisha wahamiaji wa Rohingya kwenda Bangladesh.
Karibu watu 60 wanaaminika kufariki katika ajali kama hiyo mwezii Septemba.
No comments:
Post a Comment