MPANDA
WAKAZI wa kijiji cha Milala Kata ya
Misunkumilo katika Manispaa ya Mpanda,wameilalamikia serikali kutochukua hatua
dhidi ya viboko waliopo bwawa la Milala vinavyoharibu mazao shambani na
kutishia uhai wa binadamu mara kwa mara.
Wakizungumza na Mpanda Radio wakiwemo
pia wakazi wa mitaa ya Kigamboni,Misunkumilo
na Makanyagio wamesema, madhara mengine ambayo yametokana na viboko hao
ni kuvunjika kwa ndoa zao kutokana na wanaume kuhamishia makazi yao shambani
ili kudhibiti viboko wasiharibu mazao yao.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa
Mtaa wa Misunkumilo Bw.Antipas Kalumbete ambaye pia ndiye anayekaimu nafasi hiyo
katika kijiji cha Milala,amethibitisha viboko hao kuwa tishio wa wakazi wa
maeneo hayo akisema kuwa maliasili waliandikiwa barua lakini mpaka sasa hakuna
hatua yoyote ambayo imechukuliwa dhidi ya wanayama hao.
Bwawa la milala ambalo ni miongoni
mwa vyanzo vya maji yanayotumika kwa wakazi wa Manispaa ya Mpanda inasemekana
kwa sasa lina viboko zaidi ya thelathini huku wakazi wa maeneo jirani na bwawa
hilo wakilazimika kujifungia ndani majira ya jioni wakiogopa kushambuliwa.
No comments:
Post a Comment