Mneja Viwanja na Udhibiti wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Bi. Pili Mtambalike, |
DAR ES SALAAM
Baraza la Habari
Tanzania (MCT) limesema litaanza kuwashtaki watakaovunja uhuru wa Habari
ikiwamo kuwazuia waandishi wa Habari kupata taarifa, vipigo na matukio yote ya
udhalilishaji dhidi yao.
Akizungumza katika
Mkutano Mkuu wa MCT, Ofisa Miradi wa Baraza hilo Pili Mtambalike amesema
matukio hayo yanaongeza hofu na kuwafanya waandishi washindwe kutimiza
wajibu wao kikamilifu.
Mtambalike amesema
pamoja na hatua nyingine wataanza kuwachukulia hatua ikiwamo kuwashtaki wale
watakaofanya hivyo huku akiwaasa wanahabari kutoa taarifa vinapotokea vitendo
vinavyokiuka uhuru wa habari.
Hata hivyo amesema
kwa mwaka huu zaidi ya matukio 11 yameripotiwa ikiwamo lile la Mkuu wa Mkoa wa
Dar es salaam kuvamia kituo cha TV cha Clouds.
Rais wa MCT, Jaji
Mstaafu Thomas Mihayo amesema baraza hilo lilianzisha Rejista ya Matukio
ya Uvunjaji Haki wa Habari ili kuhakikisha kila tukio linaripotiwa na
kuchukuliwa hatua.
No comments:
Post a Comment