Serikali ya mtaa wa Kampuni Kata ya
Misunkumilo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi imewaomba wataalamu wa maji
Manispaa ya Mpanda kuchunguza maji ya visima yanayotumika kwa shughuli
mbalimbali ikiwemo kunywa.
Wakizungumza na Mpanda Radio mwenyekiti
wa mtaa wa Kampuni Bw.James Simoni na
mjumbe wa serikali ya mtaa huo Bi. Flora Simoni Mpenda viongozi na wakazi wa
mtaa huo wamesema maji hayo yanaonekana na kuwa na kutu hali inayopelekea hofu
kwa watumiaji wa maji hayo kuhofia kupata madhara kiafya.
Alisema mwenyekiti Simoni Mpenda ''Wananchi
wa mtaa wa Kampuni kwa kweli wanalalamika juu ya maji ni machafu na yana rangi
kama kutu au mawese lakini sasa tunapata mkanganyiko wataalamu wa maji
wanatwambia yako salama lakini wanashindwa kunywa maji hayo''
Kwa sasa Mtaa wa kampuni wenye wakazi
zaidi ya 1680 una mabomba matatu ya visima vilivyochimbwa tangu mwaka 2015
ambapo visima hivyo vilianza kupatwa na tatizo hilo baada ya kuchimbwa visima hivyo.
Kwa upande wao wakazi wa mtaa wa
kampuni akiwemo Vitus Charles wameiomba serikali kuweka wazi taarifa ya usalama
wa maji hayo ili kunusuru afya zao.
''Tunaomba tu viongozi kutoka
serikalini waweze kulifuatilia maana mtaa huu upo nyuma kimaendeleo kwa kila
kitu hata elimu miundombinu ya barabara maji''
Mamlaka husika katika sekta ya maji
Manispaa ya Mpanda zimeahidi kuzungumzia suala hilo muda wowote baada ya kufika
mtaa wa kampuni ili kuchukua sampuli ya maji hayo na kuyapima na hatimaye kutoa
majibu ikiwa maji hayo yana madhara kwa
binadamu.
Tatizo la maji kusemekana kuwa na
kutu limekuwa rikilipotiwa pia katika maeneo mengine ya Manispaa ikiwemo mitaa
ya msasani na Tambukareli.
Habari na Issack Gerald wa mpanda
radio.
No comments:
Post a Comment