KIGOMA.
VITUO vya afya Uvinza
na Nguruka vilivyopo wilayani Uvinza Mkoa wa Kigoma vinakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo yaupungufu wa watumishi katika kada zote na hivyo kuathiri
ufanisi wakazi ambao unaweza kusababisha vifo kwa wagonjwa wanaohitaji huduma
katika vituo hivyo.
Zena Shaban na
Mapinduzi Hamisi ni baadhi ya wananchi katika wilaya ya uvinza ambapo wameiamba
mpanda redio kero wanazo kumbana nazo na mapendekezo yao kwa serikali
Stanford Chamgeni
ambaye ni mganga mfawidhi wa kituo cha afya Nguruka amesema wanakumbana na kazi
kubwa wakati wa kutoa huduma kwa wagonjwa ambapo kwa siku hutoa huduma kwa
wagonjwa 80 hadi 100 huku mganga wa Kituo cha afya Uvinza Albert Msingwa
akielezea upungufu wa majengo katika kituo chake.
Naye Mganga
mkuu wa Wilaya hiyo Albert Mumwi amekiri mapungufu hayo na kuelezea kuwa
kufikikia sasa tayari wauguzi 10 wamepatiwa ajila na tayari wamepangiwa vituo
vya kazi
Tatizo hilo la upungufu
wa watumishi limetajwa kuwa kero ya muda mrefu katika vituo vya afya wilayani
uvinza huku idadi ya wakazi ikikadiriwa kuwa 178,189 huku waganga katika wilaya
hiyo wakiwa saba na vituo vya kutolea huduma vikiwa 5.
CHANZO: ISACK ISACK
No comments:
Post a Comment