Friday, 8 December 2017

Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi inatarajia kuadhimisha miaka 56 ya uhuru wa Tanzania bara kwa kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Manispaa.

Picha ya hayati baba wa taifa mwl. J. K. Nyerere

MPANDA
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi inatarajia kuadhimisha miaka 56 ya uhuru wa Tanzania bara kwa kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Manispaa.
Akizungumza na Mpanda Radio,Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu ametaja miongoni mwa maeneo yatakayofanyiwa usafi kwa kushirikisha watumishi wa umma ni pamoja na maeneo ya stendi,Hospitali na maeneo ya soko.

Aidha Nzyungu amewataka wananchi wote kushiriki ipasavyo katika kaufanya usafi katika maeneo yao ili kuweka mazingira katika hali ya usafi.
Kwa mjibu wa Bw.Nzyungu zoezi la usafi la kesho katika maeneo yote ya Mkoa wa Katavi linaratibiwa na uongozi wa Mkoa wa Katavi.
Hatua ya kufanya usafi siku ya kesho ni utekelezaji wa agizo la rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt John Magufuli ambaye miaka miwili iliyopita aliagiza siku ya jumamosi itumike kwa ajili ya usafi nchi nzima.
CHANZO:  Mpanda radio

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...