MPANDA
Mahakama
ya Wilaya ya Mpanda imemuhukumu Omary Maganga (45) kutumikia jela
kifungo cha miaka 20 baada ya kupatikana na hatia ya kukamatwa na nyama ya
kiboko zaidi ya kilo 110.
Hukumu hiyo
Imetolewa leo Ijumaa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya
ya Mpanda, Chiganga Ntengwa baada ya kuridhika na ushahidi
uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashitaka
uliokuwa ukiongozwa na mwanasheria wa Serikali, Flaviani Shio.
Awali,
katika kesi hiyo mwendesha mashitaka huyo alidai
mahakamani hapo kuwa mshitakiwa Maganga alitenda
kosa hilo Oktoba 10 mwaka 2016 nyakati za saa 10 jioni.
Alidai
kuwa siku ya tukio mshitakiwa alikamatwa akiwa ndani ya
Hifadhi ya Taifa ya Katavi huku akiwa na nyama ya kiboko
yenye uzito wa kilo 118 ambayo thamani yake Sh 3.2 milioni.
Mwanasheria
huyo wa Serikali aliiambia mahakama kuwa mshitakiwa huyo alikamatwa na
askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi baada ya kuwa wamepata taarifa kutoka
kwa raia wema za kuwa mshitakiwa amekuwa akifanya ujangili kwenye
hifadhi hiyo.
Akisoma
hukumu hiyo Hakimu Chiganga amesema kutokana na ushahidi uliotolewa
mahakamani hapo Mahakama pasipo shaka yoyote inamtia hatiani
mshitakiwa.
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment