Mkuu wa wilaya ya mpanda mkoani katavi mheshimiwa Lilian Charles Matinga |
NSIMBO
Mkuu
wa wilaya yam panda mkoani katavi mheshimiwa Lilian Charles Matinga ameitaka
Jamii kuachana na mila kandamizi dhidi ya wanawake na watoto wa kike.
Matinga
ameyasema hayo katika kilele cha siku kumi na sita za kupinga ukatili wa
kijinsia dhidi ya mtoto wa kike na mwanamke Akielezea chanzo cha kukithiri kwa
vitendo hivyo.
Mpanda
redio imezungumza na na baadhi ya wanawake ambao wamejitokeza na kuelezea mimba
za utotoni kuwa changamoto katika
maendeleo kwa vizazi vijavyo.
Aidha
wametaja nafasi ndogo ya ushiriki wa wanawake katika maamuzi ndani ya familia
husababisha kuendelea kwa dhuruma dhidi ya makundi ya wanawake.
Maadhimisho
hayo yamefanyika katika kijiji cha ivungwe,kata ya katumba halamsahuri ya
nsimbo yakiwa na kauli isemyo Funguka ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na
watoto haumuachi mtu salama chukua hatua.
CHANZO: ALLYNANUSWE EDWARD
No comments:
Post a Comment