Na Rehema Msigwa
WAGANGA wa kienyeji wa tiba asilia wametakiwa kujisajili ili
kufuata taratibu za uendeshaji wa huduma hiyo kwa kufuata sheria.
Agizo hilo limetolewa leo na Katibu tawala wa mkoa Paul
Chagonja alipokuwa waganga wakienyeji na tiba asilia kufuatia kuwepo kwa lamri
chonganishi.
Umeuambia umati wa waganga hao kuwa wakati umefika wa
kukubali kuwa tiba asilia pamoja a madawa ya kienyeji, ni urithi ulio haribiwa
na tamaduni za kigeni, na kwamba kazi kubwa iliyobakia ni kutengeneza njia
sahihi za kihuduma ambazo zitawalinda watoa huduma pamoja na kutoa msaada kwa
wapokea huduma.
Baadhi ya waganga wakifuatilia maelekezo kutoka kwa Katibu tawala Mkoa wa Katavi Paul Chagonja (hayupo pichani) |
kwa upande wa waganga wa kienyeji na tiba asilia wamewataka
waganga ambao hawatambuliki na serikali waanze kufanya taratibu za kufanya
usajili ili kujilinda na matatizo ya
kihuduma ikiwemo mtego wa ramli chonganishi.
Maria Komba ni mmoja wa waganga wa Kienyeji amesema ipo haja ya badhi ya waganga wa kienyeji kuaacha kuwashauri
vibaya wagonjwa hasa kutokana na baadhi ya magonjwa kuhitaji uchunguzi zaidi wa
kitabibu ambao unapatikana hospitalini.
Mara kadhaa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania
imekuwa ikisimamisha huduma za waganga wa kienyeji kufuatia kuwepo kwa dhana ya
udanganyifu kwa jamii ikiwemo ramri chonganishi.
No comments:
Post a Comment